Hatimaye Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero leo hii imeweka rekodi ya kipekee baada ya uongozi wa Wilaya hiyo chini ya Mkurugenzi Mtendaji Florent Kyombo Kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Kebwe Steven Kwebe hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 141,ambazo amezikabidhi kwenye vikundi vya Wanawake na Vijana ikiwa ni asilimilia kumi ya makusanyo ya ndani ya wilaya hiyo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi Mtendaji amesema hizo ni juhudi za Wilaya mara baada ya kuboresha maeneo mbalimbali ya vyanzo vya mapato ,na kumuahidi mkuu wa mkoa kuwa wataendelea kuboresha zaidi ili ifikapo mwezi juni kuweza kumaliza kabisa kiasi kilicho bakia ambacho ni Milioni 160 , ambacho kinatakiwa kitolewe kwa vikundi hivyo vya ujasiliamali ili viweze kujiendesha katika shughuli za maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Jonas Van Zeeland amesema kuwa mshikamano na mikakati iliyopo ndani ya Halmashauri ndio imefanikisha kufikia lengo hivyo amewata viongozi wote ndani ya halmashauri kuhakikisha kuwa wanasimama imara kumalizia kiasi kilichosalia ili kutimiza malengo yao ya mwaka.
Aidha mkuu wa Mkoa amewaasa Vijana na Wanawake waliokabidhiwa fedha hizo kwenda kuzitumia kwa matumizi yaliyokusudiwa ili kuleta tija kwa jamii kwa maendeleo ya taifa.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.