Katika kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero leo Desemba 7, 2024 imefanya shughuli maalum ya kupanda miti ya matunda kuzunguka viwanja vya michezo vya Halmashauri, shughuli hiyo imeongozwa na viongozi wa wilaya kwa kushirikiana na watumishi, wananchi na taasisi mbalimbali.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mvomero, Bw. Saidi Nguya akizungumza wakati wa tukio hilo, amewashukuru Watumishi pamoja na wananchi kwa kujitokeza kushiriki katika zoezi hilo huku akisema kuwa hatua ya kupanda miti ya matunda inalenga kuunga mkono juhudi za serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kulinda mazingira, na kuhakikisha usalama wa chakula kwa vizazi vijavyo.
Katika hatua nyingine, Bw. Nguya amewataka wananchi na Watumishi kujitokeza kwa wingi kwenye kongamano la kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara litakalofanyika katika chuo cha ualimu Muhonda kuanzia saa 3.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mwl. Linno Mwageni amewashukuru Watumishi pamoja na wananchi kushiriki zoezi hilo huku akisisitiza utunzaji wa hali ya juu ili miti hiyo ikue kama inavyotarajiwa na kuleta manufaa kwa badaye.
Wakati wa tukio hilo, miti ya matunda, ikiwemo miembe, maparachichi, karafuu na karanga miti imepandwa katika eneo la viwanja vya michezo vya Halmashauri hiyo.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya 63 mwaka huu ni “Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa wananchi ni msingi wa Maendeleo yetu".
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.