• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
MVOMERO DISTRICT COUNCIL
MVOMERO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Afya
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uongozi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
    • Baraza la Madiwani
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Rasilimali Watu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Itakayo tekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti

MVOMERO KUKAGUA UTENDAJI KAZI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

Posted on: November 1st, 2024

Wilaya ya Mvomero imepanga kuanza mchakato wa kukagua utendaji kazi wa mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs) yanayofanya kazi katika Wilaya hiyo ili kuhakikisha kuwa yanafuata kanuni, sheria na malengo yaliyokusudiwa kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa Novemba Mosi mwaka huu na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mvomero, Bw. Saidi Nguya wakati akifungua Kikao kazi cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali ngazi ya Wilaya kwa Robo ya Kwanza kipindi cha Julai - Septemba 2024 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.

Katibu Tawala huyo amesema mchakato huo unalenga kutathmini na kubaini kama mashirika haya yanatimiza malengo na ahadi walizoweka kupitia maandiko yao kwa jamii na wafadhili wao huku akisisitiza kuwa ni muhimu mashirika haya kufuata miongozo iliyowekwa ili kuimarisha uwazi na ufanisi katika utoaji wa huduma na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi wa Mvomero.

"...kama ambavyo tunaikagua miradi ya Ruwasa, tunaikagua miradi ya barabara, tunakagua miradi ya shule, miradi ya hospitali, tunataka kuanze kufanya ufuatiliaji wa taasisi baada ya taasisi, shirika kwa shirika..." amesisitiza Katibu Tawala.

Aidha, ameongeza kuwa kupitia ukaguzi huu, watajiridhisha kama mashirika haya yanafanya kazi kwa uwazi na uadilifu, na kwamba rasilimali wanazotumia zinawanufaisha wananchi kama ilivyokusudiwa huku akibainisha kuwa baada ya ukaguzi huo taarifa itatolewa itakayoainisha mashirika ambayo yanatekeleza kwa vitendo maandiko ya miradi yao kwa wananchi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mwl. Linno Mwageni ameyataka mashirika hayo kutekeleza majukumu yao kwa kufuata mila na desturi za nchi ya Tanzania na kuacha kuiga tamaduni za kigeni ambazo ni kinyume maadili ya mtanzania.

Awali wakati akisoma taarifa ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Mratibu wa Mashirika hayo Wilaya ya Mvomero Bw. Azizi Msuya  amesema katika Wilaya hiyo ina Mashirika 60 ambayo yanafanya kazi, Bw. Msuya ameongeza kuwa Mashirika hayo yanatekeleza miradi mbalimbali katika Sekta za Elimu, Sheria, Kilimo, Mifugo, Afya pamoja na Mazingira.

Nao Viongozi na wasimamizi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Wilayani Mvomero akiwemo Bw. Medson ameishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kwa kutambua mchango wa mashirika hayo katika maendeleo ya Wananchi wa Wilaya hiyo, huku akitumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi na Watendaji wa mashirika hayo  kudumisha mila na desturi za nchi yetu ya Tanzania.

MWISHO.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 14, 2025
  • MAJINA YA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WALIOITWA KWENYE USAILI OKTOBA 17, 2025 October 14, 2025
  • MAJINA YA RESERVE WA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WANAOTAKIWA KWENYE USAILI KATIKA KATA October 14, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MVOMERO YAWEKA MIKAKATI YA KUFANYA VIZURI KATIKA KIPENGERE CHA USAFI WA MAZINGIRA

    August 20, 2025
  • ZOEZI LA UTOAJI FOMU ZA UTEUZI LAENDELEA KUSHIKA KASI

    August 20, 2025
  • UTOAJI WA FOMU ZA UTEUZI

    August 19, 2025
  • DC MAULID DOTTO AAHIDI KUTAFUTA ENEO KWA AJILI YA MASHINDANO YA MAGARI

    August 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kimkoa yafanyika Halimashauri ya Wilaya Mvomero
Video Zaidi

Viungo vya Haraka

  • Ukurasa wa Facebook

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira
  • Baraza la Mtihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero

    Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO

    Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348

    Mobile: +255 23 293 4348

    Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.