Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero imeibuka mshindi wa nne na kubeba Kombe kwenye ushindi wa jumla kwenye maonesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki 2024 ambayo yamefungwa na Mhe. Mizengo Pinda Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Agosti 8, 2024 katika viwanja vya Mwl. Nyerere vilivyopo katika Manispaa ya Morogoro.
Aidha, Halmashauri hiyo imepata ushindi wa nafasi ya kwanza Kimkoa na kupata Kombe. Pia, imepata ushindi katika nafasi ya Mfugaji bora na kupata cheti.
MKuu wa Wilaya hiyo Mhe. Judith Nguli ameongoza shamra shamra za ushindi huo akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Mwl. Linno Mwageni, Makamu M/kiti wa Halmashauri Mhe. Christopher Maarifa pamoja na baadhi ya Waheshimiwa Madiwani na Watumishi wa Halmashauri hiyo.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.