Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewataka wananchi Mkoani humo kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi hususan suala la wafugaji kulisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima huku akiwataka kuviachia vyombo vya sheria kushughulikia suala hilo.
Mhe. Malima ametoa kauli hiyo Juni 10, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Mtakenini kilichopo Kata ya Doma akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya barabara zilizoharibiwa na mvua.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema linapotokea suala la wafugaji kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima basi mkulima aliyelishiwa shamba lake anatakiwa kutoa taarifa kwenye Serikali ya Kijiji ili hatua za kisheria zifuatwe na kwamba asijichukulie sheria mkononi.
“...mwenye jambo lake la wakulima na wafugaji nawaomba msijichukulie sheria mkononi...” amesema Mkuu wa Mkoa.
Aidha, Mhe. Malima amebainisha kuwa Serikali haitasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote atakayejichukulia sheria mkononi.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.