Bohari ya Dawa (MSD) tarehe 5/12/2023 imegawa vifaatiba vyenye thamani ya Shilingi Milioni 500 kwa Zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ikiwa ni kutimiza azma ya Serikali ya kuhakikisha kwamba huduma za afya zinaendelea kuboreshwa na kuwapatia wananchi wake huduma bora.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika hospitali ya Wilaya ya Mvomero na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali ngazi ya Wilaya , wananchi pamoja na watumishi wa Bohari ya Dawa, viongozi walisisitiza umuhimu wa vituo vya kutolea huduma za afya kuwa na vifaa bora ambavyo vitawapatia wananchi huduma ya kiwango kinachostahili.
Awali akitoa hotuba yake kwa niaba ya Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa, Meneja wa Kanda ya Mashariki Bi. Bestia kaema alisema kuwa wameleta vifaatiba vyenye thamani ya Shilingi Millioni 500 kati ya Bilioni 1 ikiwa ni awamu ya kwanza ya ugawaji wa vifaatiba hivyo na kwamba awamu ya pili itafuata kuanzia mwisho wa mwezi Januari na mwanzo wa mwezi Februari 2024.
Pia ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero na Mkurugenzi Mtendaji Mwl. Linno Mwageni kwa juhudi anazoonesha kwenye ufuatiliaji wa dawa na vifaatiba na kwamba kwa kufanya hivyo wanawapa wananchi kupata haki ya huduma wanayostahili. Aliongeza kuwa kwa sasa ugawaji wa dawa na vifaatiba umeongezeka kwa wamu kutoka mara nne mpaka mara 6 kwa mwaka .
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.