Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) ambalo linaendesha mradi wa Mkaa Endelevu (TTCS) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) Mkoani Morogoro. Lengo likiwa ni kuhakikisha rasilimali misitu inakuwa endelevu. Mradi huo katika Wilaya ya Mvomero unatekeleza katika Vijiji vya Maharaka, Sewe Kipera, Msongozi, Ndole, Magunga, Kihondo, Diburuma, Masimba, Msolokelo na Misengele.
Akizungumza katika kikao na Waandishi wa habari kilichoitishwa na Mkurugenzi wa TFCG ili kuzungumzia manufaa ya mradi huo katika Vijiji vya Wilaya ya Mvomero, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo Bibi. Mary M. Kayowa alisema kuwa mradi umesaidia wananchi kuwa na uelewa wa uhifadhi wa mazingira katika maeneo yao, mradi huo umewawezesha wananchi kupata kipato kutokana na mazao ya misitu wanayo miliki. Pia mkaa endelevu umewawezesha wananchi kulinda mazingira yao ili yasiweze kuharibiwa, mradi umesaidia katika kupeleka watoto Shule, kufanya shughuli za kilimo na biashara nyingine.
“Kutokana na faida hizo Menejimenti imeona itenge Bajeti ya Sh. Mill 10 kwa ajili ya kuanzisha mradi katika Vijiji vingine vya Njeula na Matale, pia tumepanga kuandaa Mfuko ili wafadhili pia waweze kuchangia”.
Afisa Misitu wa Wilaya ya Mvomero alieleza kuwa Halmashauri ilianza kutekeleza mradi huo mwaka 2015 ambapo walianza na kuandaa mpango wa uvunaji na kufanya tathmini katika maeneo ya Msongozi, Misengele, Maharaka na Msolokelo na baadae Ndole, Magunga na Masimba.
Mradi umesaidia kutangaza misitu ya Vijiji Vitano katika Gazeti la Serikali GN. N0.688 ya tarehe 28.08.2020.
“Kutokana na mradi huo hali ya misitu imeboreka kulingana na ilivyokuwa nyuma, baada ya kujengewa uwezo na usimamizi bora uelewa wa jamii umeboreka”.
Vijiji vimekuwa na uvunaji endelevu kwa kupishana, kupitia mradi huo Vijiji vimeimarisha uhifadhi wa misitu. Vijiji vimekuwa vinavuna misitu yao na kuweza kuuza ili kupa mapato. Pia wamefundishwa mbinu endelevu na kutumia mapato yao wameweza kujenga huduma za kijamii za ujenzi wa madarasa, Zahanati, vyoo vya Shule na barabara. Halmashauri imeona ni muhimu kuendeleza mradi huo kwani unanufaisha jamii na kutunza misitu.
Aidha Halmashauri imetenga fedha kwa ajili ya kuanzisha mradi katika Vijiji vya Njeula na Matale na kutoa elimu ili Vijiji viweze kuchangia 10% kwa ajili ya kusaidia mradi.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.