Mradi wa Eco Schools umeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu na utunzaji wa mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa serikali na wadau wa maendeleo, unalenga kuimarisha elimu ya mazingira shuleni huku ukiboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.
Hayo yamebainishwa Disemba 2, 2024 na Meneja wa mradi huo, Bw. James Michael wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hii katika ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.
Bw. James amesema kuwa mradi wa Eco Schools unatekelezwa katika shule 57 za Msingi na Sekondari ndani ya Halmashauri hiyo na unalenga kuboresha uraia pamoja na kuboresha maisha ya watu.
Ameongeza kuwa mradi huo umejikita katika maeneo matatu ikiwemo uhifadhi wa mazingira, elimu bora na maendeleo endelevu kwa kushirikisha wazazi na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha kuwa hayo yanafanikiwa.
Kwa upande wake Afisa Elimu shule za Awali na Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mwl. Bruno Sangwa amesema Halmashauri hiyo ina shule 163 za msingi ambapo kupitia mradi wa Eco Schools umeanzisha miradi midogo midogo ambayo husaidia shule kupata fedha za kuendesha shule pamoja na upatikanaji wa chakula shuleni hivyo kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.