Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Maulid Dotto ameendelea na ziara yake ya kujitambulisha, kujua maeneo ya mipaka na kusikiliza kero za wananchi katika Kata na Vijiji vya Wilaya ya Mvomero, ambapo Oktoba 9, 2025 amefika Kijiji cha Kanga na Dihinda Kata ya Kanga akiwa ameambatana na Wataalam kutoka Halmashauri na Taasisi mbalimbali zilizomo ndani ya Wilaya ya Mvomero.
Katika mkutano huo wa hadhara, wananchi walipata fursa ya kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo tatizo la umeme hususan Kitongoji cha Kisauke, wafugaji kuingiza ng'ombe kwenye mashamba ya wakulima, ubovu wa barabara, mpaka wa hifadhi usogezwe ili wananchi wapate maeneo ya kuishi, ndege aina ya quelequelea wanakula mazao ya mpunga, barabara inayounganisha mikoa ya Pwani na Tanga itengenezwe, wanafunzi wanatembea umbali mrefu Km 4 kutoka Shule mama ya Kanga wananchi wanaomba wajengewe Shule ya mkondo, utoaji wa hati miliki za ardhi utekelezaji wake haufiki mwisho, pembejeoza kilimo zinapatikana mbali Madizini mjumbe aliomba huduma zisogezwe na mwananchi alilalamikia eneo la shamba lake kuvamiwa na mwekezaji hata akikodisha anakuja kumtishia.
Akizungumza baada ya kusikiliza kero hizo, Mhe. Dotto aliwataka Wataalam watoe majibu kwa hoja zilizowasilishwa mezani pia aliawahakikishia wananchi kuwa Serikali ya Wilaya ya Mvomero imedhamiria kusikiliza na kushughulikia kero zote kwa wakati ili kuhakikisha amani, utulivu na maendeleo vinaendelea kupatikana katika maeneo yote ya Wilaya. Alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Viongozi wa Vijiji na wananchi katika kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi.
Aidha alisisitiza kuwa Serikali ina dhamira ya dhati ya kuboresha maisha ya wananchi wa Mvomero kupitia utatuzi wa migogoro, uboreshaji wa miundombinu na upanuzi wa huduma za jamii.
Wananchi walimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kufika kusikiliza kero zao moja kwa moja na kuonesha matumaini kuwa hatua stahiki zitachukuliwa ili kupunguza changamoto wanazokabiliana nazo.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.