Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Judith Nguli amewaongoza viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala wa Wilaya ya Mvomero Ndg. Said Ngutaya kwenye uzinduzi wa Kampeni ya umezaji wa dawa kwa ajili ya kingatiba ya ugonjwa wa Usubi katika Kijiji cha Kibaoni, Kata ya Melela na kuonesha mfano kwa kumeza dawa hizo mbele ya hadhara ya mamia ya wananchi waliofika kumsikiliza kijijini hapo.
Katika zoezi hilo, Mkuu wa Wilaya amewahimiza wananchi kushiriki kumeza dawa hizo na kuondokana na dhana potofu ya kuwa dawa hizo zina madhara kwenye miili yao. Amesema dawa hizo zinamezwa na jinsia zote na kiume na kike ndio maana ameonesha mfano kwa kumeza pamoja na Katibu Tawala pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji .
Kwa upande wake, Mratibu wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele Wilayani Mvomero, Bi. Amina Saidi amewataka wananchi kumeza dawa hizo kuepukana na ugonjwa huo unaoenezwa na nzi wadogo weusi wenye uwezo wa kuruka hadi kilomita 50, hivyo ni vyema wanachi wakachukua tahadhari mapema ili kuepukana na athari za ugonjwa huo.
Alisema kuwa dawa hizo zinaweza kumezwa na watu kuanzia umri wa miaka mitano na kuendelea, isipokuwa wakinamama wakinamama wajawazito na wanaonyonyesha chini ya siku 7. Miongoni mwa dalili za ugojnwa huo ni pamoja na mgonjwa kupata upele kwenye ngozi ya mwili, uchuchukaji wa mwili ambao kwa pamoja vinaweza kusababisha upofu endapo tahadhari haitochukuliwa.
Kampeni ya umezaji wa dawa za Usubi katika Wilaya ya Mvomero zimeanza tarehe 21 Agosti na zinatarajia kukamilika mnamo tarehe 31 ya mwezi huo.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.