Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli amefanya ziara kukagua Mradi wa Umwagiliaji katika Bonde la Mgongola katika Kata ya Lukindo ili kujionea hatua ilipofikia mradi huo na kutoa maelekezo kadhaa juu ya ukamilishwaji wa mradi huo.
Mkuu wa Wilaya amemjia juu mkandarasi wa mradi huo na kuhoji kusuasua kwa ukamilishwaji wa mradi huo huku ikiwa imebakia miezi miwili tu kwa muda uliopangwa mradi huo kukamilika ufikiwe.
Amesema licha ya Rais Samia kuelekeza kiasi kikubwa cha fedha kuwapa wakulima wa Mvomero fursa ya kuwa ya kilimo , bado mradi huo unasuasua huku mradi huo ukifikia 41% pekee licha ya mkandarasi huyo kulipwa fedha na kukabidhiwa rasmi kuanza kutekeleza mradi huo kuanzia Septemba 7 mwaka 2022.
Katika ukaguzi wake Mkuu wa Wilaya amebaini kuwa mkandarasi huyo hana vifaa vya kutosha kukamilisha mradi huo, huku vifaa alivyonavyo ni duni na vibovu hivyo kuharibika mara kwa mara inayopelekea kutokamilishwa mradi kwa muda uliokusudiwa.
“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta fedha nyingi sana kuongeza thamani ya Wakulima wa Mkindo na Wilaya ya Mvomero. Bilioni 5.6 sio fedha ndogo.Kuna watu wanataka kuhujumu maendeleo kwa kukwamisha skimu hii.” Alisema Mkuu wa Wilaya wakati akizungumza na Wanakijiji wa Kijiji cha Bungoma kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.
Skimu ya Umwagiliaji ya Mgongola iliyopo kata ya Mkindo Wilayani Mvomero ni moja kati ya Skimu zilizopokea fedha jumla ya Shilingi Bilioni 15 kutoka Serikalini kumsaidia Mkulima kuwa na uhakika kwa kuvuna mazao ya kilimo ikiwemo Rudewa (7.2 Bilioni), Idete (Bilioni 2.3 ).
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.