Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Halima Okash jana amekabidhi pikipiki mbili, majokofu mawili na matanki 15 pamoja na vifaa vya kutunzia ubaridi wa Kikundi cha Wakinamama Wajasiriamali (Tushikamane Group) kutoka Kijiji cha Sokoine kilichopo kata ya Dakawa Wilaya ya Mvomero.
Akikabidhi vifaa hivyo vilivyotolewa na shirika la Heifer International, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wakinamama hao kuvitumia vifaa hivyo kwa lengo lililokusudiwaili viweze kuleta tija ikiwa ni pamoja na kuwaletea kipato ili waweze kujikwamua kiucchumi.
Mkuu wa Wilaya amelishukuru shirika la Heifer International kwa kuwawezesha vifaa hivyo wakinamama hao na kuwataka kuendelea kuwasaidia jamii nyingine inayozunguka Wilaya ya Mvomero kwani kwa kufanya hivyo kutawafanya wakinamama wengi kujishughulisha katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kuwanyanyua kiuchumi.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Heifer International Mark Tsoxo amesema kuwa wametoa vifaa hivyo kwa kikundi cha Tushikamane ili iweze kuwarahisishia shughuli zao za uchakataji na utunzaji maziwa baada ya kuwapatia mafunzo ya uelewa wa shughuli hizo na hivyo kuahidi kusaidia katika shughuli nyingine za uzalishaji mali zikiwemo za ukopeshaji wa ng’ombe wa maziwa pamoja na utoaji wa pembejeo za mifugo.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.