Mkuu wa Wilaya Mvomero Mh. Albinus Mugonya, leo amekabidhi pikipiki aina ya honda yenye thamani ya shilingi Mil. 4.5 kwa Afisa elimu kata wa kata ya Kweuma iliyopo Tarafa ya Turiani Ndg. Hamisi Iddi Hamisi kwa ajili ya ufuatiliaji wa maswala ya elimu katika kata hiyo.
Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mh. Mkuu wa Wilaya amesema kuwa kutolewa kwa pikipiki hiyo ni Imani yake kuwa kutaboresha utendaji kazi wa Afisa huyo na kuleta ufanisi katika suala zima la elimu kwani hapo awali kata hiyo ilikuwa haina chombo cha usafiri cha kumuwezesha Afisa huyo kutembelea shule zilizopo katika eneo lake na kushindwa kusimamia suala zima la kuboresha kiwango cha elimu katika kata hiyo.
Mh. Mkuu wawilaya amemtaka Afisa Elimu kata huyo kwenda kutumia usafiri huo kwa makusudi yaliyo kusudiwa na kuhakikisha anasimamia suala zima la uboreshaji wa Elimu katika kata hiyo kwani hapo awali alikuwa akishindwa kutekeleza majukumu yake na hivyo kusababisha kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa ya usimamiaji wa majukumu ya elimu na kusababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika kata hiyo.
Awali akitoa taarifa hiyo mbele ya Mkuu wa Wilaya kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Maajabu Nkanyemka, amesema tayari halmashauri imeshakabidhi jumla ya pikipiki 29 kwa Maafisa Elimu Kata katika kata 29 kati ya 30 zilizopo katikaHalmashauri hiyo na hivyo kukabidhiwa kwa pikipiki hiyo hii leo inakamilisha pikipiki 30 ambazo zote zimekabidhiwa kwa Maafisa Elimu Kata 30 wa kata zote ndani ya wilaya.
Kaimu mkurugenzi huyo amesema kuwa ni Imani yake sasa baada ya kukamilisha kugawa pikipiki zote 30 katika kata 30 kutawafanya Maafisa Elimu Kata hao kwenda kusimamia maswala ya elimu kwa ufanisi zaidi na hivyo kusababisha kupandisha kiwango cha ufaulu ndani ya wilaya na kusimamia maswala yote yanayohusu elimu.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.