Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli amewataka wananchi wa Wilaya ya Mvomero kuitumia vizuri hospitali ya Wilaya hiyo kwani ndio hospitali kubwa nayaa kisasa Zaidi kuliko zote ndani ya Wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo wakati akiongoza viongozi wa Serikali katika mapokei ya vifaatiba vyenye thamani ya shilingi Milioni 500 kwa ajili ya vitio mbalimbali vya kutolea huduma za afya vilivyotolewa na Bohari ya Dawa yaliyofanyika katika Hospitali ya Wilaya tarehe 5 Desemba 2023.
Amewataka wananchi wa Mvomero wafike kupata huduma katika katika hospitali hiyo kwani ina vifaatiba, huduma na wataalamu wa kutosha na kuwa wananchi wasiende mbali kufuata huduma za afya na badala yake waitegemee hospitali hiyo ambayo Serikali imetumia fedha nyingi ili kusogeza huduma karibu yao.
Ameongeza pia kuwa kijiografia , hospitali hiyo ipo katika barabara kuu ya Dodoma-Dar es Salaam yenye wingi wa magari na inapotokea dharura yoyote maeneo ya karibu, hospitali hiyo ndio mkombozi . “Tuna viwanda vikubwa hapa vya Mkulazi, Mtibwa na Kiwanda cha Nyama cha Nguru. Inapotokea ajali yoyote hapa ndio sehemu ya karibu ya kupata huduma za afya.”
Mkuu wa Wilaya ameongeza kuwa kwa vifaatiba ambavyo Bohari ya Dawa imeleta , huduma nyingi kwenye hospitali hiyo zitakuwa zinapatikana ambayo ni pamoja na jokofu la kuhifadhia maiti.Alisema kuwa awali maiti zilikuwa zinahifadhiwa mbali lakini sasa hakuna haja ya kwenda Manispaa ya Morogoro kwani majokofu hayo matatu yatasiadia kupatikana kwa huduma ya uhifadhi wa maiti muda wote.
Awali akitoa taarifa fupi ya mapokezi ya vifaa hivyo, Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Phillipina Phillipo ameishukuru Bohari ya Dawa kwa amesema kuwa wametenga kiasi cha shilingi Bilioni 1 na Milioni 150 kwa ununuzi wa dawa na vifaatiba na kwamba siku hiyo wamepokea vifaatiba vyenye thamani ya shilingi milioni 500 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma ya Afya Dakawa, Mlali na Mziha na Kibati pamoja na Hospitali ya Wilaya.
Akitoa shukrani zake , Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Yusuph Makunja amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwakumbuka wananchi wa Mvomero na kuwa wasipate tabu kwenda kupata huduma mbali kwani hii ndio hospitali kubwa kuliko zote ndani ya Wilaya ya Mvomero na kuwa Rais Samia amewathamini sana ndio maana amesogeza huduma bora za afya karibu yao.
Naye mbunge wa jimbo hilo Mhe. Jonas Van Zeeland amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya wananchi wa jimbo lake na kusisitiza kuwa hospitali hiyo ni muhimu sana kwenye ukanda huu na kwamba kama mbunge wa jimbo hilo atahakikisha kuwa sera ya afya inayotaka kila kijiji kuwa na zahanati, kila kata kuwa na kituo cha afya inatekelezwa na kuagiza maboma ambayo yameanzishwa na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa zahanati yanakamilika.
Hospitali ya Wilaya ya Mvomero inahudumia wananchi Zaidi ya laki 4 wa Wilaya hiyo kwa mujibu wa sense ya watu na makazi yam waka 2023.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.