Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martine Shigela ,Jana amefanya ziara Wilayani Mvomero kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani humo pamoja na kusikiliza keto za Wananchi.
Awali Mkuu huyo wa Mkoa ametembelea na kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya Dakawa na kuupongeza Uongozi wa Wilaya mpaka Kijiji kwa jinsi wanavyoonesha ushirikiano wa utekelezaji wa mradi huo.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema pindi mradi huo utakapokamilika utaleta tija kwa wananchi wa kata ya Dakawa na maeneo jirani.
Pia Mhe. Martine Shigela amewataka viongozi hao kuendeleza ushirikiano huo katika kusimamia miradi mingine ya maendeleo iliyopo katika maeneo mengine Wilayani humo .
Katika hatua nyingine Mhe. Mkuu wa Mkoa amefanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kichangani kilichopo katika Kata ya Mhonda Tarafa ya Turiani kwa lengo kusikiliza kero mbalimbali za Wananchi.
Miongoni wa kero hizo ni pamoja na bei ya chini ya zao la kokoa, upatikanaji hafifu wa maji na umeme katika Kata hiyo ,pamoja na upungufu wa nyumba za walimu na waganga katika Kata hiyo na Tarafa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa ameagiza viongozi wote walioguswa na kero hizo kuhakikisha wanazitatua kwa haraka kero hizo ili wananchi waweze kufaidi matunda ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Halima Okash amemuahidi Mkuu wa Mkoa kusimamia yote aliyoagiza na kuhakikisha yanatekelezwa kwa wakati ili wananchi wa Mvomero waweze kupata maendeleo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mvomero Mhe. Jonas Van Zeeland amesema kuwa yeye pamoja na uongozi mzima wa Wilaya ya Mvomero wamejipanga kuhakikisha wanasimamia miradi yote iliyotengewa pesa na kuhakikisha inatekelezwa kwa wakati pamoja na kutatua kero mbalimbali za wananchi Wilayani humo.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.