Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Ndg. Linno P. Mwageni amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo kutumia fursa zilizopo katika Wilaya hiyo katika kukuza uchumi na kuchochea maendeleo.
Ndugu Linno P. Mwageni ametoa wito huo wakati akizungumza na watumishi katika kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo huku akieleza kuwa Wilaya ya Mvomero imejaaliwa kwa kila kitu ikiwemo kuwa na Ardhi nzuri kwa ajili ya Kilimo, Madini, Biashara na Ufugaji.
Pia amemtaka Afisa Ardhi wa Halmashauri hiyo kutenga maeneo na kuwauzia viwanja watumishi ambapo watatakiwa kulipia kidogo kidogo ndani ya mwaka mmoja.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji, Linno P. Mwageni amewataka Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira, nao kutenga maeneo ya Msitu kwa ajili ya kutundika mizinga ya Nyuki na kuanzisha kikundi cha watumishi kwa ajili ya ufugaji wa Nyuki, pamoja na kuwataka watumishi kutunza Mali za Umma ikiwemo Ofisi zinazowazunguka.
Kwa upande wao, watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero walipokea maelekezo na maagizo ya Mkurugenzi.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.