Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Ndugu Hassani Njama Hassani amewataka maafisa mifugo ngazi ya Kata na Vijiji kukaa na kujikita Zaidi katika maeneo yao ya kazi ili kutoa huduma kikamilifu kwa wananchi.
Akizungumza katika kikao kazi kilichofanyika hapo jana katika Ukumbi wa Halmashauri kati yake na Watendaji hao,Mkurugenzi Mtendaji amesema amepata malalamiko mengi kuwa baadhi ya maofisa hao kutokukaa katika maeneo yao ya kazi na hivyo kukwamisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
Mkurugenzi huyo amesema inashangaza kuona baadhi ya Watendaji wanalipwa mishahara na Serikali lakini wanashindwa kutoa huduma stahiki kwa wananchi na wengine kutokuonekana katika maeneo yao ya kazi kwa muda mrefu,jambo ambalo linakwamisha ufanisi wa kazi.
Aidha mkurugenzi huyo ameagiza kuanzia sasa Mtendaji yeyote atakaeshindwa kuonekana katika eneo lake la kazi bila taarifa rasmi anatakiwa aondolewe kazini haraka iwezekanavyo ili kupisha wengine wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo wapewe nafasi.
“Inashangaza kuona Mtendaji au Afisa Mifugo analipwa mshahara na serikali lakini haonekani kazini,naagiza wale wote watakaoshindwa kutekeleza maagizo haya waondolewe kazini”,alisema.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi amemuagiza Mkuu wa Idara hiyo kuangalia uwezekano wa kuanza kuwalipa madeni watumishi wa idara hiyo kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ili kupunguza malimbikizo ya madeni ya watumishi hao.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.