• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
MVOMERO DISTRICT COUNCIL
MVOMERO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Afya
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uongozi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
    • Baraza la Madiwani
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Rasilimali Watu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Itakayo tekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti

MKURUGENZI INEC AWASISITIZA WAANDHISHI WASAIDIZI, WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI NGAZI YA KITUO KUZINGATIA MUDA WA KUFUNGUA VITUO VYA KUANDIKISHA WAPIGA KURA

Posted on: May 14th, 2025

Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ndg. Ramadhani Kailima ametoa wito kwa waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki ngazi ya kituo wilayani Mvomero kuhakikisha wanazingatia muda wa kufungua vituo vya kuandikisha wapiga kura ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.

Ndg. Kailima ametoa wito huo Mei 14, 2025 wakati akizungumza na washiriki wa Mafunzo ya zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura Awamu ya Pili yaliyofanyika katika ukumbi wa Prof. Kuzilwa uliopo katika Kata ya Mzumbe.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa uchelewaji wa kufungua vituo unaweza kuwakatisha tamaa wananchi na kudhoofisha hamasa ya kushiriki katika mchakato wa uchaguzi.


Aidha, ameongeza kuwa Tume ya Uchaguzi imejipanga kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa uwazi, ufanisi na kwa kuzingatia maadili ya uchaguzi, na kwamba usimamizi wa karibu katika kila ngazi ni muhimu ili kuhakikisha lengo hilo linafikiwa.


Sambamba na hilo, Mkurugenzi huyo amewasisitiza washiriki hao juu ya umuhimu wa kutunza vifaa ambavyo vinatumika katika zoezi hilo akisema kuwa vifaa hivyo vimenunuliwa kwa gharama hivyo wanapaswa kuvitunza.


Kwa upande wake Afisa Muandikishaji Daftari la kudumu la wapiga kura Jimbo la Mvomero Bi. Mary Kayowa amesema kuwa katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili Jimbo hilo litakuwa na vituo 50 ambavyo vitatumika akiongeza kuwa zoezi hilo litafanikiwa kwa asilimia 100 kwa kuwa hamasa kwa wananchi inaendelea kufanyika.


Aidha, Bi. Mary Kayowa amewataka washiriki kuwa na ushirikiano pamoja na kufanya kazi kwa weledi ili kuhakikisha kuwa malengo yaliyowekwa na Tume yanafikiwa.


Zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura kwa Awamu ya Pili linatarajia kuanza tarehe 16 hadi 22 Mei, 2025 huku likienda sambamba na kuwekwa wazi kwa Daftari la Awali.


"Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora".


MWISHO.

Matangazo

  • MAJINA YA WAANDISHI WASAIDIZI NA BVR KIT OPERATORS. February 22, 2025
  • Majina ya Waandishi wasaidizi na BVR KIT Operators February 22, 2025
  • Kuitwa Kwenye Usahili Nafasi Ya Mtendaji Wa Kijiji,Mtunza Kumbukumbu,Afisa Hesabu Msaidizi,Dereva wa Ambulance na Katibu Muhtasi. October 12, 2021
  • TENDER MVOMERO May 28, 2022
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WITO UMETOLEWA KWA WADAU, SERIKALI KUONGEZA JUHUDI KATIKA UTOAJI ELIMU YA HEDHI SALAMA VIJIJINI

    May 28, 2025
  • WAHE. MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MLIMBA WATEMBELEA MVOMERO KUJIFUNZA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI UNAVYOWAKOMBOA WAKULIMA WA KAKAO

    May 24, 2025
  • MVOMERO KUUZA UFUTA KUPITIA STAKABADHI GHALANI KUANZIA MEI 20, 2025

    May 16, 2025
  • MKURUGENZI INEC AWASISITIZA WAANDHISHI WASAIDIZI, WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI NGAZI YA KITUO KUZINGATIA MUDA WA KUFUNGUA VITUO VYA KUANDIKISHA WAPIGA KURA

    May 14, 2025
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kimkoa yafanyika Halimashauri ya Wilaya Mvomero
Video Zaidi

Viungo vya Haraka

  • Ukurasa wa Facebook

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira
  • Baraza la Mtihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero

    Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO

    Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348

    Mobile: +255 23 293 4348

    Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.