Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Hassani Njama Hassani, amewaagiza walimu wakuu wote wa Wilaya hiyo kuwa ifikapo Mei 28 atakayeshindwa kuwasilisha fedha za michango ya UMITASHUMTA atakuwa amejiondoa katika nafasi yake.
Hayo ameyasema hii leo alipofanya kikao cha pamoja na walimu wakuu hao kujadili mambo mbalimbali yahusuyo upandishwaji wa taaluma katika wilaya hiyo.
Mkurugenzi huyo amesema ni aibu kubwa kuona kuna shule 23 tu ndizo zimemaliza michango kati ya shule 149 ambazo shule 126 uchangiaji wake ni wa kusuasua hivyo amewataka walimu wakuu hao kwenda kujitathmini mpaka tarehe tajwa na atakayeshindwa kufanya hivyo mpaka ifikapo tarehe 31 atakuwa nje ya madaraka.
Pia Mkurugenzi huyo amewataka wakuu hao kwenda kusimamia nidhamu walimu walio chini yao na wanafunzi kwa ujumla kwani kuna taarifa kwamba baadhi ya walimu wanashiriki matendo yasiyo ya kimaadili na wanafunzi wanaowasimamia jambo ambalo sio maadili ya kiuwalimu.
Pia amewataka walimu wakuu kwenda kupandisha ufaulu na kuhakikisha wilaya inafanya vizurina kushika nafasi za juu kimkoa na kitaifa.
Kwa upande wake Afisa Elimu wa Wilaya hiyo Maajabu Nkanyemka amesikitishwa na kiendo cha walimu wakuu hao kushindwa kufikisha lengo la uchangiaji wa michango hiyo wakati pesa walikuwa wanazipokea kwa wakati kutoka serikalini lakini wameshindwa kuziwasilisha kwa wakati jambo ambalo linakwamisha uendeshaji wa shughuli za michezo mashuleni.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.