Mkuu wa wilaya ya mvomero, mhe. Judith nguli amesema kuwa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri imekuwa chachu katika kupambana na umaskini na kuimarisha maisha ya wananchi.
akizungumza oktoba 08, 2024 wakati wa mafunzo ya utoaji mikopo kwa kamati za mikopo wilayani humo, dc nguli ameeleza kuwa mpango huo unalenga kuleta maendeleo kwa kuwapa wananchi mitaji inayowawezesha kuanzisha na kukuza biashara ndogo ndogo.
"...kwa hiyo ili tunalolifanya tunakwenda kupambana na umaskini na kuwezesha wananchi wetu kiuchumi..." amesema mkuu wa wilaya.
Aidha amesema kuwa mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi - ccm inayoelekeza serikali kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Sambamba na hilo, mhe. Nguli ametoa wito kwa wanufaika wa mikopo hiyo kuhakikisha wanarejesha mikopo kwa wakati ili wengine pia waweze kunufaika.
Naye, kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya mvomero mwl. Bruno sangwa amesema serikali ilisitisha zoezi la utoaji mikopo ya asilimia 10 hapa nchini kwa lengo la kuja na mikakati madhubuti ya kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na mikopo hiyo kupitia vikundi vya vijana, wanawake na wenye ulemavu. Ameongeza kuwa kwa sasa serikali imetoa miongozo mipya ya utoaji mikopo hiyo.
Kwa mwaka huu, halmashauri ya wilaya ya mvomero imetenga zaidi ya shilingi milioni 600 kwa ajili ya mikopo ya vikundi, ikiwa ni sehemu ya jitihada za serikali za kuhakikisha wananchi wanainuka kiuchumi na kupambana na umasikini.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.