Wito umetolewa kwa wawekezaji hapa nchini kujitokeza kwa wingi kujenga viwanda vitakavyosaidia kuongeza upatikanaji wa sukari hapa nchini.
Hayo yamesemwa hapo jana na Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika Prof.Adolf Martin Mkenda alipofanya ziara ya kikazi Wilayani Mvomero na kutembelea kiwanda cha kuzalisha Sukari cha Mtibwa,kisha kuongea na wadau mbalimbali vikiwemo vyama vya ushirika vilivyomo Wilayani hapa.
Prof.Mkenda amesema endapo wadau mbalimbali watajitokeza kujenga viwanda na kuzalisha Sukari kwa wingi hivyo itaisaidia nchi kutokuagiza Sukari nje ya Nchi.
Mh,Waziri amesema kwa mwaka huu nchi italazimika kuagiza Sukari nje ya nchi ili kukidhi upungufu uliopo wa hitaji la Sukari hapa nchini,lakini ameahidi kuanzia mwakani nchi haitalazimika tena kuagiza Sukari nje ya nchi.
Mh.Prof.Mkenda amewataka wamiliki wote wenye Viwanda vya kuzalisha Sukari hapa nchini,kuhakikisha wanaongeza uzalishaji kwa wingi ili kufikia mwakani Sukari yote iwe inapatikana hapa nchini ni si kuagiza nje ya nchi tena.’’Nawaagiza wamiliki wote wenye viwanda vya kuzalisha Sukari ni lazima wahakikishe wanaongeza uzalishaji wa Sukari hapa nchini kwani ifikapo mwakani hatutalazimika tenakuagiza Sukari nje ya nchi na Sukari yote itapatikana hapa nchini,na atakaeshindwa kufanya hivyo hatua nyingine zitachukuliwa’’.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.