Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana ,Ajira na Wenye Ulemavu )Mhe. Prof. Joyce Ndalichako , leo amefanya Ziara Wilayani Mvomero kwa kutembelea na kukagua Machinjio ya Kisasa ya Nguru Hills ,yaliyopo Kijiji cha Wami Luhindo kata ya Dakawa, Tarafa ya Mvomero Wilayani Mvomero.
Katika ziara hiyo Mhe. Waziri amewapongeza wawekezaji wa kiwanda hicho kwa kutoa kipaumbele kwa kuajiri zaidi ya Vijana 40, ambayo tayari wameanza kufanya kazi kiwandani hapo katika hatua za awali.
Mhe. Ndalichako ameutaka uongozi wa Serikali Wilayani humo chini ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kuwahamasisha wakulima na wafugaji kufuga Kisasa na kutumia rasilimali za aridhi zilizopo wilayani humo kufuga Kisasa ili mifugo yao ipate thamani ya kununulika .
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Halima Okash amemhakikishia Waziri kuwa kwa kutambua uwekezaji huo tayari wameanza mikakati ya kuwahamasisha wafugaji kila Kijiji waliko kuhakikisha wanaacha kuchunga na badala yake wabadilishe mtazamo na kuhakikisha wanaanza kutenga maeneo na kuanza kufuga kisasa ili Mifugo iweze kupata thamani ya kununulika .
Aidha Mhe. Mkuu wa Wilaya amewata vijana kutumia fursa hiyo ya uwepo wa Machinjio Wilayani humo kwa kutafuta fursa mbalimbali za mikopo zilizopo ndani na nje ya wilaya Ili kujikwamua kiuchumi,
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.