Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatuma Mwasa, amewataka wananchi waliojenga katika Msitu wa kuni uliopo Wilaya ya Mvomero, katika maeneo ya ng’ambo ya korongo kuondoka mara moja katika eneo hilo na kutii amri iliyotolewa na Mamlaka.
Alisema hayo katika ziara ya kikazi iliyofanyika katika Kitongoji hicho baada ya kuona wananchi wamekaidi amri ya kusitisha ujenzi unaoendelea katika maeneo hayo na kuagiza Meneja wa Msitu wa Kuni, Vyombo vya Ulinzi na usalama kufanya zoezi la kubomoa nyumba zote zilizowekewa alama X na kuwataka wananchi kuwa wasikivu wanapopewa amri na Mamlaka.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Halima Okash alisema Serikali imetoa kibali kwa nyumba zipatazo 1214 zilizohakikiwa kuendelea kuwepo katika eneo hilo na kuzitaka nyumba zilizojengwa baada ya zoezi la uhakiki kuondolewa mara moja.
Mhe. Mkuu wa Mkoa alionyesha masikitiko yake kwa wananchi wa maeneo hayo kukaidi agizo la kuondoka mahali hapo ndani ya muda uliopangwa na kuwataka kutii amri hiyo mara moja.
Msitu wa Kuni ni msitu ulihifadhiwa na Serikali kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira na uoto wa asili katika eneo hilo. Msitu huo upo katika eneo hilo tangu mwaka 1954.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.