Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amefanya ziara Wilayani Mvomero katika muendelezo ya ziara anazozunguka nchi nzima kukagua maendeleo ya miradi iliyoelekezwa kuinua ustawi wa wananchi nchini.
Katika ziara hiyo, Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametembelea Skimu ya Umwagiliaji katika Kijiji cha Lukenge kata ya Mtibwa inayofadhiliwa na Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) na pia alitembelea Kijiji cha Mingo kata ya Lubungo kukagua maendeleo ya ujenzi wa kisima cha maji safi.
Katika mradi wa Skimu ya umwagiliaji Kijiji cha Lukenge unaofadhiliwa na mradi wa EBARR chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais, aliagiza ukamilishwaji wa mradi huo ndani ya muda kwani ni kipindi kirefu sana kimepita bila mradi kukamilika huku serikali ikiwa imetoa fedha kwa asilimia 100 na kuagiza uongozi wa Mkoa usimamie hili swala.
Aidha katika ujenzi wa kisima katika Kijiji cha Mingo, Mhe. Dkt. Selemani Jafo aliridhishwa na utekelezaji wake huku akitoa maelekezo kwa wataalamu kutoka Wakala wa Maji Vijijini na Mijini (RUWASA) kuhakikisha ifikapo Juni 28 mwaka huu kisima hiko kiwe kimekamilika kwa asilimia 100 ili uweze kuleta tija kwa wananchi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Kwa upande wa Kijiji cha Mingo, akiongea kwa niaba ya wananchi wa eneo hilo, Mwenyekiti wa Kijiji hiko Bw. Rashid Kibukila aliishukuru Serikali kupitia ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuwaletea mradi huo kwani ni muhimu katika usatawi wa maisha ya wananchi.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.