Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi, Mh. Angelina Mabula amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Hassan Njama kuongeza kasi ya usimamizi wa upimaji wa maeneo ya ardhi hususan maeneo ya taasisi na mashamba yaliyopo wilayani humo.
Akizungumza na uongozi wa Halmashauri hiyo hapo jana katika kikao kilichofanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya, Mh. Naibu waziri amesema kutokana na taarifa aliyosomewa inaonyesha wilaya hiyo bado ina kazi kubwa ya kufanya katika zoezi la upimaji wa ardhi ikiwamo mashamba Pamoja na maeneo ya taasisi. Hivyo kuwataka maafisa ardhi kuandaa mpango kabambe wa kuwezesha kufanikisha zoezi hilo.
Aidha Mh. Naibu waziri amewataka maafisa ardhi kuandaa mpango wa upimaji wa mashamba pori yote yaliyofutwa na Mh. Raisi na kuwasilisha kwa Mh. Waziri wa Ardhi kwa ajili ya kuwagaiya wananchi ili wayatumie kwa shughuli za kilimo na ufugaji
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo Hassan Njama amesema wameyapokea maagizo hayo ya Mh. Naibu waziri na kumhakikishia kwamba watayafanyia kazi kwa haraka iwezekanavyo ili kuhakikisha wanakamilisha mpango huo kwa muda muafaka.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.