• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
MVOMERO DISTRICT COUNCIL
MVOMERO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Afya
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uongozi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
    • Baraza la Madiwani
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Rasilimali Watu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Itakayo tekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti

MOROGORO YAJA NA MKAKATI KUSHUGHULIKIA MADAI YA WAFANYAKAZI

Posted on: May 1st, 2025

Mkoa wa Morogoro umeandaa mkakati madhubuti wa kushughulikia madai ya wafanyakazi yakiwemo madai ya likizo, uhamisho, matibabu, kukaimu, kujikimu, ajira mpya na malimbikizo ya mishahara kwa waliondolewa kazini kimakosa mwaka 2017 ili kuhakikisha kuwa wanapata stahiki zao kwa mujibu wa sheria.

Hayo yamebainishwa Mei 01, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima wakati akizungumza na Viongozi pamoja na wafanyakazi wa Mkoa huo kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) ambayo kimkoa yameadhimishwa katika uwanja wa Jamhuri, Manispaa ya Morogoro.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa Ofisi yake itafanyia kazi suala la madai ya wafanyakazi ili kuhakikisha kuwa kila mfanyakazi anapata maslahi yake ambayo yapo kwa mujibu wa sheria.

“...baada ya Maadhimisho haya Ofisi yangu itafanya kazi ya ziada kuhakikisha kuwa suala hilo linapewa uzito wa kipekee...” amesema Mkuu wa Mkoa.

Aidha, amewataka waajiri wote Mkoani humo kuweka madai ya wafanyakazi kwenye mpango na bajeti ili kulipa madai hayo huku akisisitiza kuwa madai yao si suala la utashi binafsi bali ni takwa la kisheria.

Sambamba na hilo, Mhe. Malima amewaelekeza Waajiri kwa kushirikiana na vyama vya wafanyakazi kuhuisha orodha ya madai ya wafanyakazi na kuiwasilisha taarifa hiyo katika ofisi yake.


Kwa upande wake Mratibu wa Maadhimisho ya Mei Mosi 2025 Mkoa wa Morogoro wakati akisoma Risala iliyoandaliwa na Vyama vya wafanyakazi Mkoani humo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi hapa nchini.


Pamoja na pongezi hizo amemuomba Mkuu wa Mkoa kuingilia kati madai ya wafanyakazi ili waweze kupata maslahi yao.


Sherehe za Mei Mosi 2025 zinapambwa na kaulimbiu isemayo “Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, utuletee Viongozi wanaojali Maslahi ya Wafanyakazi, Sote Tushiriki”


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 14, 2025
  • MAJINA YA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WALIOITWA KWENYE USAILI OKTOBA 17, 2025 October 14, 2025
  • MAJINA YA RESERVE WA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WANAOTAKIWA KWENYE USAILI KATIKA KATA October 14, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MVOMERO YAWEKA MIKAKATI YA KUFANYA VIZURI KATIKA KIPENGERE CHA USAFI WA MAZINGIRA

    August 20, 2025
  • ZOEZI LA UTOAJI FOMU ZA UTEUZI LAENDELEA KUSHIKA KASI

    August 20, 2025
  • UTOAJI WA FOMU ZA UTEUZI

    August 19, 2025
  • DC MAULID DOTTO AAHIDI KUTAFUTA ENEO KWA AJILI YA MASHINDANO YA MAGARI

    August 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kimkoa yafanyika Halimashauri ya Wilaya Mvomero
Video Zaidi

Viungo vya Haraka

  • Ukurasa wa Facebook

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira
  • Baraza la Mtihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero

    Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO

    Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348

    Mobile: +255 23 293 4348

    Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.