• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
MVOMERO DISTRICT COUNCIL
MVOMERO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Afya
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uongozi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
    • Baraza la Madiwani
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Rasilimali Watu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Itakayo tekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti

Makabidhiano ya Hati

Posted on: March 21st, 2019

Halmashauri ya Wilaya Mvomero imekabidhiwa yaliyokuwa majengo ya Wakala wa Barara Nchini (TANROAD) yaliyopo Kijiji cha Mvomero wilayani Mvomero ili kuwa kituo cha Afya Mvomero tarehe 21/03/2019. Majengo yaliyokabidhiwa ni pamoja na Nyumba type one iliyokuwa ikitumiwa na Mhandisi Mkazi, Nyumba type two iliyokuwa ikitumiwa na Wahandisi wasaidizi, Nyumba za Multiple, Jengo la Ofisi, Jengo la Maabara, Uzio, Kisima cha maji na Matenki ya kuhifadhia maji, Mabanda ya kupaki magari, Mabanda ya walinzi, Banda la kufulia Nguo, na Jengo la choo cha Jumuia.

Akipokea hati ya makabidhiano, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr. Kebwe Steven Kebwe amesema majengo hayo ni mazuri, na amesisitiza yatunzwe ili yadumu. Aidha katika kuimarisha utunzwaji wa majengo hayo, Dr. Kebwe amemuagiza meneja wa TANROAD kuweka vivuko maalum vya kupitishia Mifugo katika eneo hilo. Pia ameagiza huduma muhimu za Kituo cha Afya kama vile huduma ya upasuaji kama kigezo muhimu cha kituo cha Afya, viwepo katika kituo. Vile vile ameagiza thamani nyingi zilizokuwa katika majengo hayo zirudishwe ziweze kufaa katika uendeshaji wa kituo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mwl. Mohamedi Utaly amepokea hati ya makabidhiano ya majengo hayo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa na kuahidi kuyatunza ili yadumu. Pia amemsifia Mkurugenzi wa Halmashauri kuwa yupo makini na kazi yake na hivyo maagizo yatatekelezwa.

Pia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Mvomero Ndugu. Florent Kyombo amekiri kupokea hati ya makabidhiano kwa niaba ya wananchi wa Mvomero na kuhakikisha kwamba yanatoa huduma inayostahili. Akiwasilisha risala kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya amesema majengo haya yanajitosheleza kuwa na huduma mbalimbali kama ifuatavyo; Wodi ya Akina Mama wajawazito, Wodi ya Watoto, Wodi ya wanaume, Wodi ya wanawake, Chumba cha upasuaji, Jengo la Mama baba na Watoto (RCH), Maabara, Bohari ya dawa, Chumba cha ufuaji, Chumba cha CTC, Chumba cha meno, Chumba cha wagonjwa wanje na Jengo la Utawala. Ameishukuru wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Wakala wa barabara (TANROAD) kuweza kukabidhi majengo haya katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli ambayo inapambana na vifo vya mama wajawazito na Watoto. Pia ameainisha changamoto mbalimbali zinazokabili idara ya Afya ikiwa ni pamoja na; Upungufu wa watumishi, Upungufu wa gari la kubebea wagonjwa pale inapotokea dharura kwa ajili ya kwenda hospitali ya Wilaya au Mkoa, Umeme mbadala kama vile jenereta au umeme jua (Solar), Mashine ya kufulia na Vifaa mbalimbali katika chumba cha upasuaji.

Matangazo

  • VIGEZO VYA MASHARTI YA ASILIMIA 10 ZA FEDHA YATOKANAYO NA MAPATO YA NDANI September 16, 2022
  • Tangazo la Usaili wa Mahojiano Utakaofanyika 21/10/2021 October 20, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MUDA ANWANI ZA MAKAZI February 18, 2022
  • TANGAZO KUITWA KWENYE USAILI MFUMO ANWANI ZA MAKAZI March 07, 2022
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WANANCHI MVOMERO WAMSHUKURU RAIS SAMIA

    January 05, 2023
  • Watumishi wa Mvomero wajumuika kufanya usafi Eneo la Hospitali ya Wilaya

    December 07, 2022
  • Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro aagiza Wananchi kuondoka katika eneo la Msitu wa Kuni.

    November 26, 2022
  • Mradi wa Mkaa Endelevu Ulivyobadili Maisha Ya Wananchi Wa Wilaya ya Mvomero

    November 21, 2022
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kimkoa yafanyika Halimashauri ya Wilaya Mvomero
Video Zaidi

Viungo vya Haraka

  • Ukurasa wa Facebook

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira
  • Baraza la Mtihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero

    Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO

    Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348

    Mobile: +255 23 293 4348

    Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.