Mafunzo kwa Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya kata katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero yamehitimishwa huku washiriki wakisisitizwa kuwa makini katika utunzaji wa vifaa vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mafunzo hayo yalilenga kuwawezesha maafisa hao kupata uelewa wa kina kuhusu taratibu za uandikishaji, matumizi sahihi ya vifaa kama vile mashine za BVR (Biometric Voter Registration) na umuhimu wa uhifadhi wa nyaraka muhimu za wapiga kura.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Afisa Muandikishaji Msaidizi Jimbo la Mvomero Bi. Mary Kayowa amesema kuwa vifaa hivyo vimenunuliwa kwa gharama kubwa hivyo Maafisa hao wametakiwa kuwa makini katika utunzaji wake ili kuepusha uharibifu ama upotevu ambao utaathiri zoezi la uandikishaji.
"...kwa hiyo kutokuwa makini katika utunzaji wa vifaa hivi utapelekea athari kubwa katika ukamilishaji wa zoezi hili..." amesema Bi. Mary
Sambambana hilo, Afisa Muandikishaji huyo amewataka kuzingatia muda wa kufungua na kufungwa kwa vituo vya kuandikisha wapiga kura, akisisitiza kuwa vituo vifunguliwe kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.
Pamoja na hayo, Maafisa Waandikishaji wametakiwa kuhamasisha Wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la uboreshaji wa daftari ambapo zoezi hilo litaanza tarehe 01-07/3/2025
Nao, Maafisa Waandikishaji wasaidizi wamewashukuru na kuwapongeza Maafisa kutoka Tume Huru ya Uchaguzi (iNEC) kwa mada nzuri huku wakiahidi kuwa zoezi hilo litakamilika kwa asilimia 100.
"Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora"
MWISHO
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.