Mafundi, wazabuni na makundi maalumu wilayani Mvomero wamejengewa uwezo wa namna ya kutumia Mfumo wa Manunuzi kwa njia ya Kielektroniki (NeST) ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na bidhaa mbalimbali za serikali.
Mafunzo hayo yametolewa leo Septemba 20, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero yakiwahusisha makundi maalum, Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Kata pamoja na Wazabuni.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) wameandaa mafunzo hayo yakiwa na lengo la kupunguza malalamiko ya ucheleweshaji wa huduma na kuongeza uwazi katika michakato ya manunuzi.
Kupitia mfumo huo wa NeST ni fursa muhimu kwa wazabuni na watoa huduma wote hususan vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kwani mfumo huo unatoa nafasi sawa bila upendeleo.
Aidha, mafunzo hayo yatawasaidia washiriki kuelewa hatua za uandikishaji, usajili wa nyaraka, pamoja na namna ya kushiriki zabuni kupitia mfumo wa kidigitali, jambo litakaloongeza ufanisi na kupunguza gharama.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.