Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 ambaye pia na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mwl. Linno Mwageni leo Septemba 26, 2024 ametoa maelekezo muhimu kuhusu utaratibu kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakao fanyika Novemba 27, 2024.
Miongoni mwa maelekezo yaliyotolewa na Msimamizi huyo wa uchaguzi Mwl. Linno Mwageni ni pamoja na tarehe ya uchaguzi, muda na sehemu ya kuandikisha wapiga kura ambapo katika Halmashauri hiyo kutakuwa na vituo 687 vya mpiga3 na zoezi hilo litaanza Oktoba 11 - 20, 2024. sifa za mgombea pamoja na mpiga kura, Nafasi zinazogombewa, Siku ya utoaji na urejeshaji wa fomu za kugombea.
Aidha, ametaja maelekezo mengine ikiwa ni pamoja na uteuzi wa Viongozi, ukataji wa rufaa, siku na utaratibu wa kampeni za uchaguzi.
Sambamba na hilo Mwl. Mwageni ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kushiriki uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura, kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi huku akisisitiza kila mtu kufuata kanuni na taratibu zilizotolewa.
“Serikali za Mitaa, Sauti ya wananchi, Jitokeze kushiriki uchaguzi”.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.