MAANDALIZI YA NANE NANE KANDA YA MASHARIKI YAPAMBA MOTO
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya hiyo kwa maandalizi mazuri ya maonyesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki 2024.
Mhe. Nguli ametoa pongezi hizo Juni 29, 2024 mara baada ya kuwasili katika ukaguzi wa vipando katika banda la maonesho la Halmashauri hiyo huku akijionea namna mazao yalivyopandwa kwa ustadi na kuzingatia kanuni bora za kilimo. Kutokana na ukaguzi aliofanya Mhe. Judith amethibitisha kuwa hali ya vipando hivyo inaendelea vizuri.
Maadhimisho ya siku ya wakulima na wafugaji kitaifa yatafanyika Mkoa wa Dodoma Agosti 8, 2024 kwa upande wa Kanda ya Mashariki siku hiyo itaadhimishwa Mkoa wa Morogoro.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka 2024 inasema “chagua Viongozi bora wa Serikali za Mitaaa kwa Maendeleo ya kilimo, mifugo na uvuvi”.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.