Laigwenani Mkuu wa Wamaasai Mkoani Morogoro Bw.Lapan Kamunge amemuomba Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli kuelekeza kikosi kazi maalum kwa wafugaji wakorofi ambao wanakiuka sheria na taratibu za matumizi ya ardhi.
Bw. Lapan ametoa ombi hilo Oktoba 07, 2024 wakati wa Mkutano wa Mkuu wa Wilaya na wafugaji kutoka kata tatu za Kifugaji uliyofanyika katika Mnada wa Mkongeni uliyopo Wilayani Mvomero.
Laigwenani huyo ameeleza kuwa baadhi ya wafugaji hao wamekuwa wakisababisha migogoro ya ardhi kwa kuingiza mifugo kwenye maeneo yasiyoruhusiwa, hali inayosababisha uharibifu wa mazingira na migogoro kati ya wafugaji na wakulima hivyo amemuomba Mkuu huyo wa Wilaya kukielekeza Kikosi kazi hicho kushughulika na Wafugaji hao ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Aidha, amesema kikosi kazi hicho kitasaidia kudhibiti hali hiyo na kuimarisha uhusiano kati ya wafugaji na jamii zingine kwa kufuata sheria zinazohusu matumizi ya ardhi na uhifadhi wa mazingira.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.