Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mvomero imekipongeza na kushukuru Kiwanda cha Sukari Mtibwa kwa juhudi zake za kusaidia wananchi kwa kurejesha mto Diwale kwenye mkondo wake wa asili, hatua inayolenga kuboresha mazingira na kuwaondolea adha ya mafuriko wakazi wa eneo hilo.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo, Machi 19, 2025 Mwenyekiti wa Kamati ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Judith Nguli amesema juhudi za kiwanda hicho ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya sekta binafsi, Jamii na Serikali katika kutunza mazingira na kulinda vyanzo vya maji pamoja na kuokoa maisha ya watu.
"...ujio wetu huu tumekuja kwa ajili ya kutoa shukrani kwa kazi kubwa inayoendelea hapa kwenye mto Diwale ...Kampuni hii ya Mtibwa imebeba dhamana ya kutusaidia sisi Serikali tunasema asante..." Amesema Mkuu wa Wilaya.
Aidha, amesema kuwa wakazi wanaoshi karibu na mto huo wamekuwa wakiathirika na mafuriko kutokana na mto huo kuacha njia yake, hivyo kitendo cha Kampuni ya Mtibwa kurudisha mto kwenye mkondo wake ni msaada mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.
Sambamba na hilo, Mhe. Nguli amesema kuwa Serikali imeandaa mpango mkakati wa muda mrefu wa kuboresha maeneo yote yenye changamoto ya mto kuhama kwenye mkondo wake ili kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kuwa salama wakati wote hususan kipindi cha mvua.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya imetoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kushirikiana na serikali na jamii katika kutekeleza miradi kama hiyo ya kuwasaidia wananchi.
Kwa upande wake, mwakilishi wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa Bw. Moses Tenda amesema kuwa mradi huo ni sehemu ya wajibu wao wa kusaidia jamii inayozunguka kiwanda hicho. Aidha, amesema mradi huo utaendela hadi mwezi Aprili mwaka huu, huku akibainisha kuwa Kampuni ya Mtibwa itaendelea kutoa msaada kwa wananchi pale ambapo inahitajika.
Pamoja na hayo, Bw. Moses ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ambayo yamewavutia wadau wa maendeleo pamoja na wawekezaji mbalimbali hapa nchini kufanya shughuli
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.