Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mvomero, Florent Kyombo amewaagiza Waratibu wa Elimu kata na Walimu Wakuu kuhakikisha kwamba wanaongoza maadili ya kazi kwa walimu chini ya usimamizi wao ili kuboresha elimu na kuboresha kiwango cha utendaji katika wilaya.
Alisema hayo katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ambao uliwakutanisha pamoja Waratibu elimu Kata na Waalimu Wakuu ambao ulikuwa na lengo la kuboresha kiwango cha elimu na kuongeza utendaji kazi.
Mkurugenzi aliwahimiza kuitisha mikutano kwa lengo la kuleta ustawi wa sekta ya kitaaluma na kusisitiza juu ya maadili ya kazi katika maeneo yao.
Kyombo alisisitiza kuwa ili waweze kufanya mkakati kuwa halisi, Waratibu na Waalimu Wakuu wanapaswa kudumisha nidhamu kwa walimu waliopo chini yao na kushughulika na matatizo ya wanafunzi
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.