Kikao cha kamati ya Ushauri ya Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero (LAC) kimefanyika Machi 11, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Jailos Msigwa.
Kikao hicho kilijadili taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya jamii na ya hifadhi ya misitu Asilia ya Uluguru na Mkingu, miradi hii inafadhiliwa na Mfuko wa Uhifadhi wa Milima ya Tao la Mashariki (EAMCEF).
Lengo la miradi hii ni kuwainua wananchi kiuchumi pamoja na kuhamasisha utunzaji wa mazingira na misitu ambapo Jamii inayozunguka Hifadhi za Mazingira Asilia ikiwemo Mkingu na Msitu wa Ulugulu wanawezeshwa miradi mbalimbali ya kiuchumi ili waachane na shughuli zinazotegemea misitu ikiwemo uchomaji wa mkaa na kuni kama sehemu ya kujipatia kipato.
Baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na Mradi wa uboreshaji wa Kuku wa kienyeji kwa jamii inayozunguka Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Mkingu, Mradi wa Kilimo bora cha Alizeti, Mradi wa Uandaaji wa Mpango wa matumizi bora ya Ardhi, Mradi wa Uhifadhi wa Mazingira na Vyanzo vya Maji katika maeneo yanayozunguka Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Msitu wa Ulugulu, Mradi wa ufugaji bora wa Samaki na Kilimo cha Vanila pamoja na ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.