Ukarabati wa Kituo cha Afya Kibati wilayani Mvomero ambao umekuwa ukiendelea kwa miezi kadhaa sasa unaelekea ukingoni na unakaribia kukamilika .
Mkurugenzi Mtendaji (W) Mvomero, Ndg. Florent Kyombo akiambatana na Mganga Mkuu (W) Ndg. Aziz Msuya pamoja timu ukarabati wa kituo hicho walipita kuangalia hatua ilipofikia ujenzi huo ili kuhakikisha unakamilika ndani ya muda uliopangwa ili kuboresha huduma za afya kwa jamii.
Akiwasilisha taarifa za ujenzi kwa Mkurugenzi, msimamizi wa ukarabati wa kituo hicho Bw. Jumanne Shigela alisema kwamba ujenzi umekamilika kwa asilimia 82 na kwamba kwa sasa wamebakiza umaliziaji wa baadhi ya miundombinu kama mashimo ya maji taka pamoja na kondo la nyuma na kwamba wanategemea baada ya wiki kadhaa ujenzi utakuwa umekamilika kwa asilimia 100.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Florent Kyombo alipongeza juhudi zao na kuagiza timu hiyo kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa miundombinu iliyobaki ndani ya muda kwani Serikali tayari imeleta fedha kwa ajili ya ujenzi huo kwani kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakisubiri kusogezewa karibu huduma bora za afya.
Kituo cha Afya Kibati ni moja kati ya vituo 183 nchini kote ambavyo vimepokea fedha kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ukarabati miundombinu na kuboresha utoaji huduma ya afya kwa jamii. Kituo hicho kinategemewa na wananchi wa Kibati wilayani Mvomero pamoja na wilaya za karibu kama Kilindi
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.