Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Judith Nguli amezindua rasmi kampeni ya kitaifa ya utoaji wa matone ya vitamini A na dawa za minyoo kwa watoto walio chini ya miaka 5 akisisitiza kuwa ni hatua muhimu katika kuhakikisha watoto wanakua kwa afya bora na kuepuka udumavu.
Uzinduzi huo umefanyika Juni 20, 2025 katika Hospitali ya Wilaya ya Mvomero ukihusisha mamia ya wazazi waliowaleta watoto wao kupata huduma hiyo.
Akizungumza na wananchi, Mhe. Nguli amesema utoaji wa vitamini A husaidia kuongeza kinga ya mwili kwa watoto, huku dawa za minyoo zikisaidia kupambana na magonjwa ya tumbo yanayoathiri afya na maendeleo ya mtoto.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wazazi kushiriki kikamilifu katika kampeni hiyo inayolenga kuwafikia watoto wenye umri wa miezi 6 hadi miaka 5 ambayo inatolewa katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo amesema utoaji wa matone ya vitamini A pamoja na dawa za minyoo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM 2020/2025 ambayo inaelekeza Serikali kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Dkt. Phillipina Phillipo amesema kampeni hiyo inatekelezwa kwa siku 30 ambapo ilianza tarehe 1 mwezi huu katika vituo 75 vya kutolea huduma za afya.
Kampeni ya utoaji wa vitamini A na dawa za minyoo hufanyika mara mbili kila mwaka mwezi wa 6 na 12 kuanzia tarehe 1 hadi 30 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Lishe na Afya ya Mtoto.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.