Uwepo wa Kampeni ya Tutunzane Wilayani Mvomero imetajwa kuwa mwarobaini wa kupunguza ama kuondoa kabisa migogoro ya wakulima na wafugaji hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa Julai 26, 2024 na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) alipotembelea shamba la malisho la Bw. Karaita ikiwa ni ziara yake ya siku moja Wilayani humo.
Waziri Ulega amebainisha kuwa Kampeni hiyo inatoa fursa kwa wafugaji kumiliki ardhi kwa ili kupanda malisho kwa ajili mifugo yao na kujenga miundombinu ya maji hali hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji kwani hakutakuwa na mfugaji anaenda kulisha mifugo yake kwenye mashamba ya wakulima.
"...lakini hili jambo lazima litapakae nchi nzima..." amesema Waziri Ulega.
Aidha, Waziri Ulega amewapongeza Wafugaji waliopokea kwa mikono miwili kampeni hiyo ambapo zaidi ya wafugaji 370 wamepata hati miliki za ardhi huku akiwataka wafugaji wengine kujiunga katika Kampeni hiyo.
Sambamba na hilo, Mhe. Ulega akiwa katika Mnada mpya wa Mkongeni amewataka viongozi wa kisiasa Wilayani humo kuyasema mazuri yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya minada kama huo wa Mkongeni.
Waziri huyo ametembelea Mnada mpya wa Mkongeni, mashamba ya malisho pamoja na kiwanda cha nyama cha Nguru Hills.
MWISHO
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.