KAMATI YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI BUNDUKI
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Bunduki unaotekelezwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kupitiia mradi wa SEQUIP.
Akizungumza Februari 20, 2024 Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Denis Londo wakati wa ukaguzi wa miradi ya elimu Wilayani Mvomero, amesema Kamati imeridhishwa na Uongozi wa Shule ya Sekondari Bunduki kwa jinsi ilivyowajibika katika usimamizi wa mradi huu na aliwapongeza walimu wanaofanya kazi katika Shule hiyo kwa kujitoa licha ya mazingira magumu wanayopitia ikiwemo umbali wa maeneo wanayokaa hadi kufika Shuleni.
“tunaondoka na picha ya Bunduki kuwa ni Bunduki kweli kweli”. Hivyo Mwenyekiti alisema
Kamati pia imeupongeza Uongozi wa Shule kwa kuwa na Mwalimu wa kujitolewa wa somo la Kiingereza kutoka nchini Norway ambae amekuwa akiwafundishi wanafunzi hao na kufanya wanafunzi hao kuwa na interaction ambazo zinasaidia kuongeza uelewa.
Katika hatua nyingine Kamati imemtaka Diwani wa Kata hiyo Mhe. Prosper Mkunule afanye kikao na wananchi kuhamasisha kuleta wanafunzi Shuleni hapo ili kuongeza idadi ya wanafunzi kwani elimu ni bure na kwa idadi ya walimu tisa kwa wanafunzi 185 waliopo shuleni hapo ukilinganisha na maeneo mengine yaliyopo mbali na barabara Bunduki ina nafuu.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Mwl. Linno P. Mwageni amesema Halmashauri imepokea Sh. Million 30,000,000 kwa ajili ya umaliziaji wa Maabara ya Fizikia, Kemia na Baiolojia na kwamba majengo hayo yamekamilika na kuanza kufanya kazi.
Aidha, Mkurugenzi huyo ameipongeza Serikali ya Awamu ya sita kwa kutenga Bajeti kwa ajili ya umaliziaji wa maabara hizo ambazo zimekuwa chachu kwa wanafunzi kujifunza masomo ya Sayansi na kufanya mazoezi kwa vitendo.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata hiyo ya Bunduki Mhe. Prosper Mkunule ameshukuru kwa ushirikiano unaotolewa na Mhe. Mbunge na Viongozi wa Halmashauri katika kipindi cha utekelezaji wa mradi. Pia aliomba Kamati itakapokwenda Wizarani waangalie kwa jicho la kipekee kiasi cha fedha kinacholetwa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi kuwa na uwiano sawa kwa Kata za mjini na Kata za pembezoni, hali inayopelekea ugumu katika kutekeleza miradi hiyo.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.