Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Mvomero imepongeza ubunifu wa mradi wa bwawa la samaki uliopo katika Kituo cha Mafunzo ya Kilimo na Mifugo kilichopo eneo la Makao Makuu ya Wilaya.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndg. Michael T. Jaka aliyekuwa ameambatana na Wajumbe wa Kamati hiyo na Wataalam wa Halmashauri
katika Ziara ya ukaguzi wa miradi iliyofanyika mwezi wa Julai tarehe Nne mwaka huu.
Mwenyekiti Ndg. Michael Jaka aliwapongeza watumishi wa Halmashauri hiyo kwa kufanya kazi kwa ubunifu na weledi katika taaluma zao.
Ujenzi wa bwawa la samaki uligharimu kiasi cha Shilingi za Kitanzania Tshs. 10,020,000/= ambazo ni fedha za mapato ya ndani ukiwa na lengo la kuinufaisha Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kuongeza mapato na kutoa mafunzo ya ufugaji wa samaki kwa wananchi.
Mradi wa bwawa la samaki ulianza kwa idadi ya vifaranga 240 aina ya sato. Bwawa lake Lina uwezo wa kuzalisha samaki 480 na kuchukua muda wa miezi mitano hadi saba kwa uvunaji wa samaki ambao watakuwa tayari kwa matumizi ya chakula.
Aidha Kamati ya Siasa ilifanya ukaguzi wa miradi mingine ya ujenzi wa Machinjio iliyopo Kata ya Mvomero, ujenzi wa Mnada mpya wa Mikongeni uliopo Kijiji cha Milama, na ujenzi wa Wodi ya wanaume katika Hospitali ya Wilaya.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.