Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero leo Februari 10, 2025 imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya elimu na afya katika Kata za Mgeta, Mlali na Dakawa kwa lengo la kujiridhisha na utekelezaji wake pamoja na kutoa maelekezo kwa wahusika ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Ziara hiyo imehusisha ukaguzi wa miradi ya ujenzi ikiwemo ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, Bweni moja na matundu 13 ya vyoo katika shule ya Sekondari Mgeta, vyumba viwili vya madarasa yaliyojengwa kwa nguvu ya wananchi katika shule ya msingi Mkuyuni katika Kata ya Mlali. Pia Kamati hiyo imetembelea zahanati ya kijiji cha Milama iliyopo katika Kata ya ya Dakawa.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mhe. Christopher Maarifa, kwa niaba ya wajumbe wa kamati hiyo ameutaka uongozi wa shule ya sekondari Mgeta kuhakikisha kuwa viti na meza kwa ajili ya wanafunzi vinapatikana.
"...msitake vyombo viwafuatilie sijui PCCB au nini hatujafikia huko...mfanye mnavyoweza muhakikishe vitu vyetu vyote vipo ndani..." amesema Mhe. Maarifa.
Aidha, Kamati hiyo imetembelea na kukagua ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa katika shule ya Msingi Mkuyuni yaliyojengwakwa nguvu za wananchi na hatua iliyofikiwa ni kupaua.
Katika hatua nyingine, Kamati hiyo imekagua jengo la Zahanati ya kijiji cha Milama na kumuagiza Mhandisi wa Halmashauri hiyo kufanya tathmini ya gharama zitakazo hitajika ili kufanya ukarabati wa zahanati hiyo pamoja na ujenzi wa zahanati mpya.
MWISHO
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.