Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imewashauri Watendaji wa Halmashauri kuwashirikisha wananchi kuchangua maeneo ya kupeleka miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ili kuleta tija kwa watumiaji.
Hao yamesemwa Februari 20, 2024 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Dennis Londo wakati wa ukaguzi wa miradi ya elimu ya Shule za awali, Msingi na Sekondari Wilayani Mvomero.
Mhe. Londo amesema Kamati haijaridhishwa na baadhi ya maamuzi ya watu wachache ya kuhamisha miradi bila ya kuwashirikisha wananchi wa maeneo husika ambao ndio walengwa na watumiaji wa miradi hiyo. Mradi huo umebadilishiwa eneo la awali lililokuwa ijengwe Shule hiyo eneo la Makao Makuu ya Kata Homboza na ujenzi wake kuhamishiwa Kijiji cha Manza.
“Nitoe wito kwa Watendaji kuwa wazalendo na kuweka maslahi ya wananchi. Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa kwa Watanzania ni jukumu letu kufanya kazi kwa maslahi ya wananchi wetu”. Amesema Mwenyekiti wa Kamati.
Aidha, Mwenyekiti huyo amesema Kamati haijafurahishwa na kuomba msamaha kwa niaba ya Serikali kuruhusu ramani itumike katika ujenzi, Halmashauri kusaliti maamuzi yetu kwa kubadilisha eneo. Kamati inataka kujua hatua zilizochukuliwa na Mkoa kwa kwenda kuomba msamaha kwa wananchi wa Homboza.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mwl. Linno Mwageni amesema mradi huo umebadilishiwa eneo la awali la Kijiji cha Homboza na kujengwa Kijiji cha Manza kutokana na eneo la awali kutokuwa na kiwanja na eneo hilo kuwa na miinuko mikubwa hali iliyopelekea Timu ya Wataalam kutoka TAMISEMI kutoridhia eneo la awali na kuagizwa litafutwe eneo lingine.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.