Jumla ya kaya 6172 za wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF III) Wilayani Mvomero wamepokea kiasi cha shilingi Mil. 288,888,000/= awamu ya 25 tangu mpango uanze 2015 kutoka serikalini na kuzigawa katika vijiji 73 vilivyomo wilayani humo.
Mratibu wa kunusuru kaya maskini (TASAF III) Wilayani Mvomero Mahija Mdoe, amesema katika awamu hii zoezi la uhailishaji limeenda vizuri na fedha zote zilifika kwa walengwa licha ya changamoto ndogondogo zilizojitokeza.
Amezitaja baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na hali ya Jiografia ya Wilaya kutawanyika hivyo inasababisha fedha kuchelewa kufika kwa walengwa kwa wakati. Hivyo kulazimu kutumia usafiri wa pikipiki na kusababisha gharama za uendeshaji kuwa kubwa.
Mratibu ameiomba serikali kuboresha miundo mbinu ya barabara ili kusaidia kufikisha fedha za walengwa kwa wakati. Pia ametaja changamoto nyingine ni baadhi ya walengwa kutokuwa na elimu juu ya ujasiriamali, hivyo kusababisha walengwa hao kutumia fedha zao tofauti na matarajio.
Kwa upande wake Afisa ufuatiliaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini Wilayani humo, Khalidi Mweta amesema kuwa mapokeo ya wananchi waliowengi ni mazuri. Aidha amesema uhitaji wa walengwa kuwepo kwenye mpango ni mkubwa kwani mabadiliko yalioanza kuonekana kwa baadhi ya wanufaika ni makubwa.
Pia amesema changamoto kubwa ni uhitaji mkubwa wa wananchi wengi kuwa na sifa za kuwepo kwenye mpango katika vijiji vipya na vile vya awali.
Katika hatua nyingine, Afisa Ufuatiliaji huyo ameiomba Serikali na TASAF Makao Makuu kuharakisha zoezi la utambuzi kwa vijiji vipya na vya awali ili kuwafikia walengwa wote katika vijiji vyote Wilayani humo na Tanzania kwa ujumla.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.