Wizara ya Fedha kupitia mafunzo yaliyotolewa na Maafisa wasimamizi wa fedha imeiasa jamii kuwa na malengo mahususi kabla ya kwenda kukopa fedha kwenye taasisi zinazotoa huduma ndogo za kifedha ili kuzitumia fedha hizo kulingana na malengo waliyojiwekea.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika Agosti 23, 2024 katika bwalo la Polisi Wami Dakawa Bi. Grace Samwel ambaye ni Afisa Msimamizi wa fedha kutoka Wizara hiyo ameitaka jamii kuwa na malengo na mikopo wanayochukua katika taasisi za kifedha.
“...usikope tuu kwa sababu unakopa, kopa ukiwa na malengo nataka kiasi Fulani cha pesa...” amesema Bi. Grace.
Aidha, amewataka kwenda kukopa kwenye taasisi ambazo zimesajiliwa na kupata leseni ya kuendesha biashara ya ukopeshaji kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) au zilizosajiliwa na Halmashauri ambapo taratibu na masharti ya utoaji wa mikopo hiyo imewekwa wazi.
Nao wananchi waliopata elimu hiyo ya fedha akiwemo Bi. Veronica Urioa amewashukuru waendeshaji wa mafunzo hayo huku akiwashauri wananchi wenzake kuwa na utaratibu wa kuwekeza kwenye taasisi zinazotambulika ikiwemo mfuko wa UTT AMIS huku akibainisha kuwa uwekezaji huo unafaida
.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.