Idara ya Kilimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero imetekeleza maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima aliyoyatoa Oktoba 27, 2024 wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu (Kazi Maalum) Mhe. Kapt. Mstaafu George Mkuchika kwa kutoa mafunzo ya kilimo bora cha nyanya kwa wakulima wa Kata ya Doma.
Novemba 09, 2024 Wataalam wa Idara hiyo ya Kilimo imefanya mkutano na wananchi Kijiji cha Maharaka na kutoa elimu hiyo ambayo inalenga kuongeza uzalishaji na ubora wa zao la nyanya, ambalo limekuwa chanzo muhimu cha kipato kwa wakulima wa Doma. Mafunzo hayo yamejikita kwenye mbinu bora za kilimo, ikiwemo matumizi sahihi ya mbolea, mbegu bora, na udhibiti wa magonjwa ya mimea.
Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya hiyo, Bw. Mohammed Longoi amesema kuwa programu hii itasaidia wakulima kuongeza tija na ubora wa mavuno yao, hivyo kuboresha kipato chao na kuchangia kwenye uhakika wa chakula katika Mkoa wa Morogoro. Hii ni hatua muhimu katika kufikia lengo la Mkoa la kuwa na kilimo endelevu na chenye tija kwa maendeleo ya jamii.
Mafunzo hayo yanaendelea na yanatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta ya kilimo cha nyanya katika Wilaya ya Mvomero.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.