Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mwl. Linno Mwageni ametoa agizo kwa mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika Kata ya Mkindo kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa wakati uliopangwa.
Mwl. Linno ametoa agizo hilo alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi huo Januari 16, 2025 huku akisisitiza umuhimu wa kuheshimu muda wa utekelezaji wa mradi huo.
“...ikifika tarehe 30 mwezi wa kwanza nikija nikute mabadiliko makubwa kwa sababu mkataba unaisha mwanzoni mwa mwezi wa tatu..." amesisitiza Mwl. Linno.
Aidha, Mkurugenzi huyo amewataka wajumbe wa kamati ya ujenzi wa shule hiyo kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi ili aweze kukamilisha kwa wakati.
Mradi huo ambao unagharimu shilingi milioni 528,998,424.00 unajumuisha vyumba nane (8) vya madarasa, jengo moja (1) la Maktaba, jengo moja (1) la Tehama, Jengo la Maabara ya Kemia, Baiolojia na Fizikia pamoja na jengo la utawala.
MWISHO
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.