Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mwl. Linno Mwageni ameipongeza Idara ya Afya katika Halmashauri hiyo kwa kuanza matumizi ya mafumo wa kielektroniki wa ukusanyaji taarifa na mapato GoTHoMIS katika Zahanati na Vituo vya Afya.
Mwl. Mwageni ametoa pongezi hizo leo Septemba 17, 2024 wakati akifungua mafunzo ya mfumo huo wa GoTHoMIS yanayofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo yanayo lenga kuwajengea uwezo wahudumu wa afya katika utendaji kazi wao wa kila siku.
Mkurugenzi huyo amesema kwa sasa teknolojia imerahisisha utendaji kazi wa watumishi hao ambapo kazi zingine zinafanyika kupitia simu janja (Smart phones), hivyo ameipongeza idara ya afya kwa kuamua kutumia mfumo huo katika utoaji wa huduma za afya kwa wananchi huku ukisaidia kukusanya mapato pamoja na taarifa za wateja.
“…kwa hiyo mimi niipongeze idara kwa kuamua kuishi kidigitali…” amesema Mkurugenzi.
Aidha, amebainisha kuwa ili zoezi hilo lifanikiwe ni muhimu kuwa na ushirkiano pamoja na ubunifu ili kuongeza kasi ya utoaji huduma kwa wananchi. Pia, amesema ofisi yake itahakikisha kuwa kwenye maeneo yenye changamoto ya umeme yanapata mfumo wa umeme wa jua ili kufanikisha zoezi hilo.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt. Philipina Philipo amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Serikali ya kuzitaka zahanati na vituo vya Afya vinakusanya mapato yake kupitia mfumo huo wa GoTHoMIS.
Dkt. Philipina ameongeza kuwa mfumo huo utasaidia kupata kumbukumbu na takwimu sahihi za wateja wanaohudumiwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.