Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Judith Nguli, amewakaribisha wawekezaji kuwekeza katika kilimo cha malisho ya mifugo wilayani humo ili kusaidia kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji pamoja na kuinua sekta ya mifugo.
Mhe. Nguli ameyasema hayo Februari 24, 2025 kwenye kikao cha wadau wa kampeni ya tutunzane mvomero kilicholenga kupitia utekelezaji wa kampeni hiyo kwa awamu ya pili kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Akizungumza katika kikao hicho, DC Nguli ameeleza kuwa uwekezaji si kujenga viwanda na maghorofa bali hata kuwekeza kwenye kilimo cha malisho ya mifugo pamoja kujenga miundombinu ya maji na kwamba uwekezaji huo utasaidia kuhakikisha mifugo inapata chakula cha kutosha mwaka mzima, hivyo kupunguza uhamaji wa wafugaji na kuepusha migogoro ya ardhi.
"...kwahiyo nitumie nafasi hii niwaalike wawekezaji hao kuja kutusaidia kuwekeza kwenye masuala ya malisho..." amesema Mkuu wa Wilaya.
Aidha, amesisitiza kuwa serikali iko tayari kuunga mkono juhudi za wafugaji ambao wameamua kujitoa kulima malisho ili kuhakikisha kuwa changamoto ambayo wafugaji wengi imekuwa ikiwasumbua hususan ya kukosa malisho na maji inapungua ama kumalizika kabisa.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.