Zoezi la upigaji kura kuchagua Viongozi wa Serikali za Mitaa za Mitaa likiendelea Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Judith Nguli, amepiga kura kuchagua Viongozi wa Serikali ya Kijiji na Kitongoji katika kituo cha Kanisani mapema leo huku akihimiza wananchi wote kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo muhimu la kidemokrasia.
Akizungumza mara baada ya kupiga kura, Mhe. Nguli amesema mchakato wa upigaji kura katika kituo hicho unaendelea kwa utulivu, huku wananchi wakizingatia taratibu zilizowekwa.
Zoezi la upigaji kura linaendelea katika maeneo yote hapa nchini ambapo vituo vya kupiga kura vinatarajiwa kufungwa Saa 10 jioni huku serikali ikisisitiza umuhimu wa kudumisha amani.
MWISHO
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.