Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli ameahidi kushughulikia tatizo la mawe makubwa yaliyopo barabara inayounganisha Kijiji cha Lukunguni na Luwale ambayo kwa muda mrefu yamekuwa kikwazo kwa wananchi wa eneo hilo.
Akizungumza Oktoba 9, 2024 wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kijiji cha Lukunguni, DC Nguli amesema serikali itachukua hatua za haraka kuhakikisha mawe hayo yanapasuliwa na kuondolewa, ili kuboresha hali ya barabara na kuwezesha usafiri kuwa wa uhakika.
"...tupeni wiki mbili nawaomba sana tunakuja kupasua yale mawe..." amesema Mkuu wa Wilaya
Mhe. Nguli ameeleza kuwa kazi hiyo ya kupasua mawe itaanza mara moja na itatekelezwa kwa ushirikiano kati ya serikali na wananchi wa eneo hilo. Pia amesisitiza umuhimu wa ushirikiano huo ili kufanikisha azma ya kuboresha miundombinu ya barabara kwa manufaa ya jamii nzima
Barabara ya Lukunguni - Luwale ni moja ya njia muhimu kwa usafiri na biashara katika Kijiji hicho na kuondolewa kwa mawe hayo kunatarajiwa kurahisisha shughuli za uchumi katika eneo hilo.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.